Polisi Yawanasa Wanaolaghai Watu Kuwaunganisha Freemason

Polisi Yawanasa Wanaolaghai Watu Kuwaunganisha Freemason


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasilano (TCRA), wamekamata na kuwahoji watu 27 kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbalimbali ya kimtandao, ikiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Kamanda wa Polisi kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakipiga simu na kusambaza ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wakidai pesa imetumwa kimakosa, hivyo irudishwe, wengine wanadai wanasafisha nyota ili kupata utajiri na kuwaunganisha na kitu wanachodai ni Freemason.


"Wakati mwingine wanawadanganya watu kuwa wameshinda na kupata gawio kutoka kampuni mbalimbali za simu na wengine hujifanya maofisa wa serikali kwa kudai kwamba wanatatua shida za watumishi wenye matatizo, suala ambalo huishia kuwaibia pesa kwa njia ya mtandao," amesema Kamanda Muliro.


Amesema baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa wakiwa na jumla ya simu 41 na line za simu 88 za mitandao mbalimbali zenye usajili tofauti na kueleza kuwa watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad