Simba SC ya Madame C.E.O Barbara Gonzalez (@bvrbvra), kila timu ndani na nje ya nchi ilikuwa inaogopa kukutana nayo, kwani kwa Mkapa hutoki na kwenu ukizubaa utapigwa nyingi, Uongozi ulikuwa imara sana, Wachezaji wakawa na hari ya juu ya kuipambania timu, mashabiki walikuwa wakimiminika viwanjani hadi wengine wanakosa tiketi, makampuni yakamiminika kujitangaza, hadi Serikali ikaweka "Visit Tanzania" kwenye uzi mzuri wa Simba, ujenzi wa Uwanja wa timu Bunju ulikuwa kasi mno.
Mara Michuano yenye hadhi ya Juu Afrika 'AFL' ikaja kuzinduliwa Tanzania tena na Rais wa FIFA, Rais wa CAF, na Mzee Arsene Wenger, wakati tunapongeza wizara na Klabu ndipo tukaja kujua kuwa Madame C.E.O ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuja kwa mashindano hayo hapa nchini, muda huo alishafanyiwa figisu kitambo wala hayuko Simba tena, mkasema eti anatumia pesa za Klabu kwa mambo yake binafsi n.k
Siku hizi watu hawajielezi sana kuwa ni wazuri kwako, hadi ukiwapoteza na ukakutana na watu wabaya ndipo utagundua kuwa ulipoteza mtu wa thamani mno, baada ya mambo kwenda vibaya Simba SC inamkumbuka Madame C.E.O na kutumia muda mwingi kumshawishi arejee, kwa taarifa nilizonazo ni kwamba mazungumzo yanakwenda vizuri hadi sasa, anarejea kuirejesha Simba katika nafasi yake, sio kushiriki Kombe la Shirikisho bali kuitafuta nusu Fainali Klabu Bingwa Afrika.
Mimi naitwa @deustanzania