Simba Walipeleka Kibegi Mlima Kilimanjaro, Yanga Baba Lao, Wapeleka Kombe


Simba Walipeleka Kibegi Mlima Kilimanjaro, Yanga Baba Lao, Wapeleka Kombe
Timu ya wananchi Yanga SC , Juzi ilianza Safari ya kulipeleka kombe la ubingwa wao wa 30 wa Ligi kuu juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro.Kombe hilo lilipita kwenye vituo kadhaa na hatimaye leo limefika kileleni

Safari ya kombe hilo ni sehemu ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ,lakini pia wamelipeleka kombe hilo kileleni kama utani kwa wapinzani wao Simba SC

Ikumbukwe kabla ya Ligi kuanza Simba walipeleka “kibegi” kileleni na kufanya uzinduzi wa jezi , Yanga wamefanya comeback wakisindikiza na ujumbe unaosema “muda wa kupeleka vitu vya maana kileleni”

Wote wametangaza utalii lakini upande wa tambo swali nakupa wewe mdau, Kibegi na Kombe nani ameliteka soko?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad