Simba Watulie, Waepuke WATU Wanaotaka Kuwachonganisha Wanasimba na Mo Dewji...


Simba Watulie, Waepuke WATU Wanaotaka Kuwachonganisha Wanasimba na Mo Dewji...

Inabidi ifike kipindi, kama hatuwezi kuwa wanamichezo wenye maono basi tuwe binadamu wenye aibu. Kuna namna inataka kufanywa iaminike kwamba Mo hana msaada na Simba. Kwamba Mo hana haki ya kuzungumzia kuhusu faida na hasara za Simba. Kwamba Mo ni mtu aliyekuja Simba juzi ikiwa inameta meta na hana nia njema nayo. Hii picha ni ya miaka 22 nyuma. Sina haja ya kukuambia uangalie kifuani mwa jezi ni nani alikuwa anasupport timu. Hapo hakuna social media, hakuna WhatsApp channel, hakuna kibakuli. Hii ni support iliyokuwa inatolewa si kwa lingine lolote zaidi ya mapenzi kwa Simba ambayo Mo amekuwa nayo.

Naomba nikuulize: kiongozi yupi kwenye menejimenti ya Simba ya sasa hivi alikuwa anatoa hela zake kuisupport Simba miaka 22 iliyopita? Au ni rahisi tu kuipenda simba hii ambayo sasa ni tamu? Kwa muktadha tu - wakati picha hii inapigwa CEO wa sasa wa Simba Imani Kajula alikuwa meneja wa masoko benki. Mbali kabisa na mipira. Huyu ndiye leo hii awe anaipenda simba kuliko Mo? Try Again hakuwa Simba wakati huo. Mangungu hakuwa Simba wakati huo. Wote walikuwa busy na mambo yao mengine. Lakini mtu mmoja ndiye alikuwa bado na imani na Simba. Mtu huyo ni Mo kupitia METL.

Yaani ni sawa na mtoto uliyemlea tangu ana mwaka mmoja mpaka anatimiza miaka 22 leo hii apate marafiki wanaomwambia “huyu hakupendi kuliko sisi tunavyokupenda”😂😂 Inachekesha kidogo.

Rai yangu kwa wapenzi wote wa Simba, watulize akili. Hata hii njaa ya mafanikio waliyonayo ni matokeo ya kazi ya muda mrefu sana. Na safari ya Simba ya mafanikio mpaka imefika hapa haikuwa kazi ndogo! Simba mpya imeanza kusukwa 2018 na Mo. Ever since, zaidi ya bilioni 50 zimewekwa! Ever since, bajeti imepanda kutoka bilioni 3 mpaka bilioni 20. Robo fainali za Africa mara 5, ubingwa wa ligi mara 4, na mengineyo mengi!

Narudia, wanasimba watulize akili, waepuke wapigaji. Waepuke “marafiki” wanaotaka kumchonganisha Simba na Mo. Amewafikisha hapa, atawafikisha wanapotaka kwenda. Huu ndio wakati wanasimba kumlinsa Mo kuepuka wanaowatumia waandishi wa habari kumchafua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad