Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa taarifa ya mwenedo wa hali ya hewa katika msimu wa Kipupwe utakaoanza mwezi Juni hadi Agosti ,hali inayoonyesha maeneo mengi ya nchi yatakumbwa na baridi ,upepo mkali na wa wastani hali inayoweza kusababisha mlipuko wa magonjwa ya homa ya mapafu, macho na magonjwa ya mifugo.
Taarifa hiyo imeonyesha hali ya joto la bahari bahari inatarajiwa kuwa ya wastani hadi chini ya wastani ikiashiria kuambatana na mvua chache za La Nina, TMA imeshauri mipango na shughuli za kijamii zizingatie taarifa hizo na kuwakumbusha wananchi na wadau kufuatilia hali ya hewa.
Kufuatilia taarifa hiyo, umejipangaje na familia kwa ujumla kuchukua kuchukua hatua na tahadhari ili kujiepusha na matokeo hasi ya hali hiyo ya hewa, au hatua gani zilichukuliwe kupunguza madhara?