Taarifa Muhimu Kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB), Fedha Kuanza Kutoka Mei 20




Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema Wanafunzi wanufaika wa mikopo yao watapatiwa malipo ya Fedha za Kujikimu (Chakula na Malazi) kwa Robo ya Nne kuanzia Jumatatu, Mei 20, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa #HESLB, Dkt. Bill Kiwia ametoa tamko hilo baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai asilimia kubwa ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (#UDSM) wamezuiwa kufanya mitihani kwa kutokamilisha malipo ya Ada, akidai wamekwama kwa sababu wengi wanategemea malipo ya Bodi yawasaidie kulipa Ada

Aidha, HESLB imesema katika Mwaka wa Masomo 2023/2024, Serikali imetenga Tsh. Bilioni 786 kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa Wanafunzi zaidi ya 220,000 wanaosoma Shahada na Stashahada mbalimbali katika Taasisi za Elimu nchini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad