Tanzania Yatajwa Sehemu Salama Kwa Uwekezaji

 

Tanzania Yatajwa Sehemu Salama Kwa Uwekezaji

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imesema Tanzania ni Sehemu Salama ya Uwekezaji hasa ule wa Viwanda kutokana na Utashi wa Kisiasa Uliopo, ikiwemo uwepo wa mazingira yanayovutia Wawekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe wakati akizindua Kiwanda cha Saruji kilichojengwa katika eneo la Vikindu Wilaya ya Mkuranga, ambacho kinatajwa kuwa cha Pili kwa Ubora Barani Afrika, huku kikiwa cha Kwanza katika Ukanda wa Jangwa la Sahara.


"Matokeo ya kiwanda hiki maana yake ni kwamba Saruji hii itakwenda kuzalishwa nchini, kwa hiyo miongoni mwa Manufaa yake ni kwamba, Saruji hiyo itatumika hapa hapa nyumbani na itaokoa kiasi cha fedha ambazo zilikuwa zikitumika kuagiza hii Saruji nje ya nchi" amesema Naibu Waziri Kigahe

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad