TMA Wafunguka: Kimbunga Hidaya Kimepoteza Nguvu



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” unaonesha kuwa kimepoteza nguvu yake kwa kiasi kikubwa wakati kikiingia nchi kavu katika kisiwa cha Mafia.

Aidha, mawingu ya mvua yaliyokuwa yakiambatana na kimbunga hicho yamesambaa katika maeneo ya kusini mwa nchi hususan katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na maeneo jirani na kuweza kusababisha vipindi vya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo.

Kwa mfano kituo cha hali ya hewa cha Kilwa Masoko (Lindi) kimeripoti mvua ya jumla ya kiasi cha milimita 200.8 kwa kipindi cha saa 6 zilizopita ikiwa ni kiwango kikubwa sana ukizingatia kuwa wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa kituo cha Kilwa Masoko ni milimita 96.6 tu.

TMA inatoa wito kwa wote wanaojihusisha na shughuli
mbalimbali bahari kuchukua tahadhari kubwa na pia kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri na huku wakichukua tahadhari.Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” unaonesha kuwa kimepoteza nguvu yake kwa kiasi kikubwa wakati kikiingia nchi kavu katika kisiwa cha Mafia. Aidha, mawingu ya mvua yaliyokuwa yakiambatana na kimbunga hicho yamesambaa katika maeneo ya kusini mwa nchi hususan katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na maeneo jirani na kuweza kusababisha vipindi vya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo. Kwa mfano kituo cha hali ya hewa cha Kilwa Masoko (Lindi) kimeripoti mvua ya jumla ya kiasi cha milimita 200.8 kwa kipindi cha saa 6 zilizopita ikiwa ni kiwango kikubwa sana ukizingatia kuwa wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa kituo cha Kilwa Masoko ni milimita 96.6 tu. TMA inatoa wito kwa wote wanaojihusisha na shughuli mbalimbali bahari kuchukua tahadhari kubwa na pia kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri na huku wakichukua tahadhari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad