TMA yatahadharisha upepo mkubwa tena

 

TMA yatahadharisha upepo mkubwa tena

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali unaofikia km 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2, ambayo yanatarajiwa kukumba kwenye baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani (visiwa vya Mafia), Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


Taarifa ya TMA waliyoipakia kwenye Mtandao wao wa istagram Leo Mei 10, 2024, imeeleza kuwa athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuathiri baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad