Treni ya Mwendokasi ( SGR) Kutoka Dar es salaam Mpaka Dodoma Kuanza Safari Tarehe Hii


Treni ya Mwendokasi ( SGR) Kutoka Dar es salaam Mpaka Dodoma Kuanza Safari Tarehe Hii


Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema safari ya Treni ya Mwendokasi ( SGR) kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma inatarajiwa kuanza July 25,2024.


Mbarawa amesema hayo baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya SGR kipande cha Dar es salaam na kujiridhisha kuwa treni hiyo itaanza kwakuwa maandalizi yanaendelea vizuri “Nimekagua miundombinu ya madaraja na vivuko pamoja na treni kazi inakwenda vizuri na July 25,2024 tunatarajia kuanza safari ya Dar es salaam mpaka Dodoma”


Waziri Mbarawa amesema nauli ya treni hiyo itakuwa rafiki kwa kila Mtanzania na kila Mtu ataweza kusafiri kuanzia daraja la kwanza mpaka daraja la tatu na katika kuhakikisha safari ya treni hiyo inaanza bila kuwepo changamoto Mbarawa amesema kuanzia mwezi June itaanza safari ya Dar es salaam mpaka Morogoro na mifumo ya tiketi itakuwa tayari na kutoa wito kwa Watanzania kuanza kusafiri kwa treni hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad