Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania Wafungwa



Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umefungwa kwa siku mbili kutokana na ukosefu wa mtandao wa intaneti iliyoathiri nchi kadhaa za Afrika Mashariki.


“Kwa sababu ya huduma duni za mtandao kote nchini, ubalozi hautafunguliwa kwa umma,” ubalozi ulisema kwenye chapisho kwenye X (zamani Twitter) siku ya Jumatatu.

Ubalozi huo umeahirisha miadi yote ya konsula kwa siku ya Jumanne na Jumatano hadi mambo yatakapotengamaa.

Ubalozi huo, hata hivyo, utaendelea kupatikana kwa makusanyo ya visa na kushughulikia kesi za dharura zinazohusisha raia wa Marekani.

Mtandao uliyopotea tangu Jumapili asubuhi, umesababisha umeathiri huduma za intaneti nchini Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda.

Tathmini ya kampuni ya ufuatiliaji wa mtandao ya NetBlocks siku ya Jumatatu ilionyesha kuwa Tanzania imeathirika zaidi na kukatika kwa huduma za intaneti.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad