UTEUZI: Rais Samia Afanya Uteuzi Mpya.....

UTEUZI: Rais Samia Afanya Uteuzi Mpya.....


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali leo May 29,2024 ambapo amemteua Dkt. Mursali Ally Milanzi kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Mipango ya Kitaifa ambapo kabla ya uteuzi huu Dkt. Milanzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Kitaifa katika Tume ya Mipango.


Rais Samia amemteua pia Dkt. Lorah Basolile Madete kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Ubunifu wa Biashara ambapo kabla ya uteuzi huu Dkt. Madete alikuwa Meneja wa Idara ya Uchumi Benki Kuu ya

Tanzania, Tawi la Mwanza.


Rais Samia pia amemteua Dkt. Linda Ezekiel kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Menejimenti ya Utendaji na Tathmini ambapo kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, President’s Delivery Bureau (PDB).


Katika hatua nyingine Rais Samia amemteua Alban Mark Kihulla kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), kabla ya uteuzi huu Bw. Kihulla alikuwa akikaimu nafasi hiyo huku pia akimteua Prof. Najat Kassim Mohamed kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), kabla ya uteuzi huu Prof. Najat alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo (Mipango, Utawala na Fedha), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).


Rais Samia amemteua Bernadetta Nagonyani Ndunguru kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Bernadetta ni Mkurugenzi wa Mafunzo Mstaafu, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad