Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na Jonathan Caulkins kutoka Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon, umebaini kuwa matuminzi ya bangi yameongezeka nchini Marekani yakipiku matuminzi ya unywaji wa pombe.
Utafiti huo ulibaini kuwa watu milioni 17.7 wameripotiwa kutumia bangi kila siku huku watu milioni 14.7 wakitajwa kutumia pombe kila siku za maisha yao.
Mabadiliko hayo yanaonesha ongezeko kubwa la matumizi ya bangi kwa mara 15 tangu mwaka 1992 huku ikiripotiwa kuwa kwa siku zijazo idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka zaidi ya sasa.