Yanga Yafikisha 'Unbeaten' 25 Ligi Kuu

 

Yanga Yafikisha 'Unbeaten' 25 Ligi Kuu

Young Africans SC ni timu ya makombe na rekodi, hilo halina ubishi kabisa kwani ukiangalia orodha ya timu zenye mataji mengi ya Ligi Kuu Tanzania, utaikuta yenyewe pale juu huku msimu huu tukielekea kubeba ubingwa wa 30.


Achana na makombe ambayo yamekuwa ni kama utamaduni wetu kuyabeba, ishu hapa ni rekodi ambazo tumeendelea kuziweka katika michuano ya Ligi Kuu ya NBC tangu msimu uliopita.


Rekodi mpya ni kucheza mechi 25 mfululizo na kushinda zote wakiwa wenyeji, yaani hakuna sare wala kupoteza wanapokuwa uwanja wa nyumbani, wanatembeza vichapo pekee.


Kumbuka rekodi hiyo inakuja baada ya kutoka kuweka rekodi ya kucheza mechi 49 mfululizo bila ya kupoteza ‘Unbeaten’ iliyohitimishwa Novemba 29, 2022. Katika Ligi Kuu ya NBC, hakuna timu yenye unbeaten 49 kuizidi Young Africans.


Jana katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar walioshinda goli 1-0, ndiyo ulikuwa ushindi wa 25 mfululizo ndani ya Ligi Kuu ya NBC tangu mara ya mwisho tulipotoka sare ya goli 1-1 Oktoba 2022 dhidi ya Simba.


Tangu hapo, msimu wa 2022/23 Yanga walicheza mechi 12 mfululizo nyumbani na kushinda zote huku wakifunga magoli 30 na kuruhusu 4, clean sheet zikiwa 9.


Matokeo ya mechi hizo haya hapa; Yanga 1-0 KMC, Yanga 4-1 Singida Big Stars, Yanga 2-0 Mbeya City, Yanga 1-0 Prisons, Yanga 3-0 Polisi Tanzania, Yanga 3-0 Coastal Union, Yanga 1-0 Ihefu, Yanga 1-0 Ruvu Shooting, Yanga 2-0 Namungo, Yanga 3-1 Geita Gold, Yanga 5-0 Kagera Sugar na Yanga 4-2 Dodoma Jiji.


Baada ya hapo, msimu huu Yanga wamecheza mechi 13 nyumbani na kushinda zote, wakifunga magoli 33, wameruhusu 5, huku clean sheet zipo 9.


Haya hapa matokeo ya mechi hizo; Yanga 5-0 KMC, Yanga 5-0 JKT Tanzania, Yanga 1-0 Namungo, Yanga 3-2 Azam, Yanga 2-0 Singida Fountain Gate, Yanga 4-1 Mtibwa Sugar, Yanga 1-0 Dodoma Jiji, Yanga 2-1 Mashujaa, Yanga 5-0 Ihefu, Yanga 1-0 Geita Gold, Yanga 2-1 Simba, Yanga 1-0 Coastal Union na Yanga 1-0 Kagera Sugar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad