AFRIKA KUSINI: Chama Tawala ANC Chakubali Kuunda Serikali ya Umoja Baada ya Kushindwa

AFRIKA KUSINI: Chama Tawala ANC Chakubali Kuunda Serikali ya Umoja Baada ya Kushindwa


 AFRIKA KUSINI: Chama Tawala cha African National Congress (#ANC) kimekubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kupoteza idadi kubwa ya viti vya Ubunge


Akitoa taarifa hiyo baada ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama (NEC), Rais Cyrill Ramaphosa amesema “Tumeridhia kuvialika Vyama vya Siasa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo ndio njia bora ya kuipeleka mbele Nchi yetu”


Ameongeza kuwa lengo la Serikali hiyo itakuwa ni kuhakikisha yanapatikana majibu ya kero zinazowakabili Wananchi ikiwemo tatizo kubwa ukosefu wa #Ajira, Gharama za Maisha na Kukuza Uchumi


ANC ambacho kilikuwa na kawaida ya kupata zaidi ya 60% katika Chaguzi, ilianza kushuka mwaka 2019 kwa kupata 57.5%, na katika Uchaguzi wa Mei 29, kilipata 40.18% ya Kura zote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad