'Anna' wa Juakali Aamua Kuokoka, Adai Kufanya VITU Kwa Akili yake Hawezi

 

'Anna' wa Juakali Aamua Kuokoka, Adai Kufanya VITU Kwa Akili yake Hawezi

Msanii wa Filamu nchini Godliver Gordian, 'Anna' wa juakali amesema kuwa ameamua kumtumikia Mungu baada ya kuona kwa akili zake hawezi,anahitaji msaada wa Mungu.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Anna amesema amefanya mengi kwa akili zake na kuona mambo hayaendi hivyo, anamuomba Mungu awe msaada wake.


"Nikimwambia mtu kwa sasa amtumikie Mungu hatanielewa kabisa ila Kuna mapito akipitishwa atamtumikia bila kulazimishwa. Nimeamua kumtumikia Mungu na kumtukuza kutokana na alivyonipigania. Nilifanya vitu vingi kwa akili zangu nikaona siwezi baada ya kupitia sehemu mbaya akaniokoa.


"Nimeshapitia na kwa sasa nimeamua kumtumikia Mungu tangu aingilie kati maisha yangu. Namtukuza kwa kuwa amenisaidia mengi na ametenda makuu kwangu," amesema Anna.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad