Chanzo cha Mgomo Kariakoo ni Kurudishwa Kwa Kikosi Kazi


Chanzo cha Mgomo Kariakoo ni Kurudishwa Kwa Kikosi Kazi

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo , Martin Mbwana amezungumzia kuhusiana na taharuki inayoendelea katika soko la kariakoo kuhusu mgomo wa Wafanyabiashara uliotangazwa kufanyika kesho June 24,2024 ambapo amesema kero kubwa inayopelekea malalamiko ya Wafanyabiashara ni baada ya TRA kurejesha vikosi kazi vya kukusanya kodi na kufuta VAT bila kutoa taarifa kwa Wafanyabiashara na kuja kulimbikizia Watu kodi.


Akiongea na @AyoTV_ Mbwana amesema amewasiliana na Waziri wa Biashara na Viwanda akiwa Jijini Dodoma ambapo alimtaka azungumze na Waziri wa Fedha ili kujadiliana njia za kusitisha mgomo huo ambapo amesema kesho watakaa Kikao cha Mawaziri hao, Bodi ya Kariakoo pamoja na TRA, kwa ajili kupata ufumbuzi wa kina kuhusiana na suluhisho la mgomo huo.

 

Mbwana amesema chimbuko la mgomo huo lilianza baada ya sintofahamu kati ya Wafanyabiashara na TRA ambao wanatumia njia mbalimbali za kuwakandamiza wafanyabiadhara.


Amesema kero kubwa inayosemekana kuwa ni changamoto na kuleta mgomo huu katika Soko la Kariakoo ni TRA  kurudisha enforcement kubwa zaidi kuliko ya awali iliyozuiliwa na Waziri Mkuu “Maagizo ya mara ya mwisho ya Waziri Mkuu yalisimamisha enforcement hizo za TRA na kuagiza njia nzuri na sahihi ya kukusanya kodi kwa makubaliano”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad