Diarra Ataja Sababu ya KULIA ushindi Dhidi ya Azam

 

Diarra Ataja Sababu ya KULIA ushindi Dhidi ya Azam

Kipa namba moja wa Yanga, Djgui Diarra ameitaja fainali ya Kombe la FA kuwa ni moja ya mchezo wake bora ndani ya misimu yake mitatu aliyoitumikia timu hiyo huku akimtaja Mohamed Mustafa kuwa kikwazo.


Yanga imetwaa taji lake la tatu la FA msimu huu dhidi ya Azam FC kwa penati (5-6) mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex Kisiwani Zanzibar.


Akizungumza na Mwanaspoti, Diarra alisema dakika 120 walizocheza uwanjani zilikuwa ni mara mbili kutokana na ugumu aliokuwa nao langoni licha ya kutokuwa na mashambulizi mengi lakini alikuwa anatumia akili kubwa kuwaelewesha mastaa wenzake ili wamalize kazi.


“Nimecheza fainali tatu za FA msimu wa kwanza dhidi ya Coastal Union tulicheza dakika 120 na kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalti 4-1, wa pili dhidi ya Azam FC mechi ilichezwa Tanga na Keneddy Musonda aliimaliza mapema kabisa dakika ya 16,” alisema na kuongeza;


“Msimu huu umekuwa bora na mgumu kuwahi kutokea dakika 120 bora na za kupambana kwa pande zote mbili umahiri na ubora wa kipa wa Azam FC Mohammed Mustafa ulinipa mtihani mgumu kuwaelewesha wenzangu ni namna gani wanatakiwa wafanye ili kumfunga.” Alisema.


Diarra amesema alimsoma kipa huyo na kubaini kuwa alikuwa anacheza na saikolojia za mastaa wake hivyo alifanya kazi kubwa kuhakikisha anazungumza na wachezaji wenzake ili kutumia akili wakati wa kupiga penalti.


“Haikuwa rahisi kukosa penalti mbili za mwanzo kwa wachezaji wenzangu niliamni wengi wametoka mchezoni na kuamini mechi imekwisha hivyo nikawa na kazi ya ziada kuzungumza na wenzangu kwa vitendo nafurai mambo yakabadilika na sasa sisi ndio mabingwa mara tatu mfululizo,” alisema na kuongeza;


“Nilikuwa na furaha sana juzi furaha yangu ilinifanya niishi maisha ya Yanga ndani yangu ni timu ambayo imenijengea upendo mkubwa kuanzia wachezaji na mashabiki zangu nilipopata hisia hizo ndio chanzo cha mimi kulia kwa furaha.” Alisema Diarra.


SIRI YA UBORA


Akizungumzia ubora wake ndani ya misimu mitatu huku akishindwa kumpiku Ley Matampi wa Coastal Union, Diarra alisema msimu huu ulikuwa bora na wa ushindani kutokana na idadi ya makipa wa kigeni kuongezeka.


“Hakuna nilichopoteza kwani nimefanya kama nilivyofanya misimu miwili nyuma nimeiosaidia timu yangu kutetea taji kuzidiwa cleen Sheet na Matampi ni sehemu ya changamoto ya ubora wa wapinzani lakini kazi yangu nimeifanya kama inavyotakiwa,” alisema na kuongeza;


“Matampi na makipa wengine wageni msimu huu walikuwa bora wamenipa changamoto sina budi kusifia kile walichokifanya kila mmoja kwa wakati wake ameipambania timu yake na kila mtu kavuna alichokipanda tukutane msimu ujao.” Alisema Diarra.


Kipa huyo ambaye alitwaa tuzo ya kipa bora wa mwaka misimu miwili mfululizo tangu ametua Yanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad