EURO 2024 Kanuni Mpya ya Mpira Inatumika, Hakuna Mchezaji Kuongea na Refa


EURO 2024 Kanuni Mpya ya Mpira Inatumika, Hakuna Mchezaji Kuongea na Refa


EURO 2024 itakua tofauti kidogo,katika michuano hii kwenye masuala ya uamuzi, kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ya Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya (UEFA), Roberto Rosetti ni kwamba, makapteni wa timu pekee ndio wanaruhusiwa kuzungumza na mwamuzi wakati wa mechi na si vinginevyo.

Vilevile ikitokea timu kapteni wao ni golikipa kama ilivyo kwa Italaia (Gianluigi Donnarumma) na Slovenia (Jan Oblak), benchi la ufundi la timu hizi litatakiwa kumtaarifu mwamuzi kwamba ni mchezaji gani wa ndani ambaye atakuwa akiwasil-iana naye wakati wa mechi, kwa sababu itakuwa ngumu kwa mwamuzi kwenda na kurudi kuzungumza na kipa.

Mbali ya hili, pia kutakuwa na utaratibu wa mwamuzi kuelezea mashabiki juu ya uamuzi alioufanya baada ya kwenda kwenye VAR.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad