Form Six Waliochaguliwa JKT Ruksa Kuripoti Kambi yoyote ya Karibu




Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesikia kilio cha wazazi na walezi wa wahitimu wa kidato cha sita ambao waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kwa mujibu wa sheria, lakini hawajaripoti baada kuwaruhusu kwenda kwenye kambi zilizo karibu na makazi yao.

Hivi karibuni Mkuu wa JKT, Meja Jenerali, Rajabu Mabele alitoa wito kwa wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa lazima mwaka 2024.

Vijana hao walitakiwa kuripoti katika kambi walizopangiwa wakiwa na vifaa walivyoainishiwa, kuanzia Juni Mosi, 2024 hadi Juni 7, 2024.

Leo Juni 22, 2024, Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jenerali Rajabu Mabena aliwatangazia vijana wote walioitwa katika mafunzo hayo ya lazima lakini hawajaripoti kambini hadi sasa, kuripoti mara moja katika kambi za karibu.

Amesema uamuzi wa kuwataka kuripoti katika makambi yaliyo karibu badala ya yale waliochaguliwa awali, unatokana na jeshi hilo kupokea maombi kutoka kwa wazazi na walezi ya kuomba kubadilishiwa kambi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad