H Baba Amwangukia Harmonize tena

H Baba Amwangukia Harmonize tena


Miaka miwili iliyopita, msanii nguli wa Bongo Fleva, H Baba alijitoa kwenye familia wa Konde Gang chini ya Harmonize na kuhamia Wasafi chini ya Diamond Platnumz.


Baada ya kuondoka kwa Harmonize, H Baba alitoa maneno mengi machafu na udhalilishaji kwa Harmonize huku akimsifia Diamond Platnumz kwa kumuomba msamaha na kumsujudia miguuni.


Lakini baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo tofauti na matarajio yake, familia ya Diamond imekuwa ikionyesha kutokuwa na muda nae, kumnyima upenyo wa kula chungu kimoja.


H Baba ameamua kurejea kwenye kambi yake ya awali ya Konde Gang na bila hiyana Harmonize amempokea kwa mikono miwili baada ya kumpigia magoti na kujutia maamuzi yake ya kuisaliti kambi ya Konde Gang.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad