HATIMAYE Mwakinyo Ashinda Ubingwa WBO Kwa TKO Dhidi ya Bondia Mghana


HATIMAYE Mwakinyo Ashinda Ubingwa WBO Kwa TKO Dhidi ya Bondia Mghana


Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ameshinda Ubingwa wa WBO kwa TKO kwa kumpiga Bondia Mghana Patrick Allotey aliyeshindwa kuendelea na pambano round ya pili akidai ameumia bega.


Pambano hilo lilipangwa kuchezwa usiku wa

kuamkia June 01,2024 kati ya Mtanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya Patrick Allotey la kuwania Ubingwa wa Afrika mkanda wa WBO na lilishindwa kufanyika kwasababu Mwakilishi wa WBO Afrika, Samir Captain hakufika ulingoni.


Mwakinyo alisema sababu iliyokwamisha pambano “Kuna changamoto kidogo imejitokeza, inabidi pambano letu sisi lisimamiwe na

Rais wa WBO ambaye yupo Dar es salaam lakini kuna changamoto zilitokea katika utafutaji wa malipo yake kutokana na changamoto ya kupatikana kwa Dola, Mzee ametafutwa na hapatikani kwenye simu, tumejiandaa vya kutosha na tuna utayari wa kupigana lakini kinachoweka uzito ni hicho, nina hamu ya kukata kiu ya Mashabiki wangu lakini nikifanya hivyo ni makosa na itaharibu kabisa carrier yangu”


Baada ya kushindwa kufanyika usiku wa kuamkia June 01,2024, pambano hilo limerudiwa tena usiku wa kuamkia leo June 02,2024 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad