Hatma ya Kocha Mgunda SIMBA Bado Haijajulikana, Simba Wafuata Kocha Huku

Hatma ya Kocha Mgunda SIMBA Bado Hajajulikana, Simba Wafuata Kocha Huku

 INAELEZWA kwamba Uongozi wa Simba SC utaachana na Kaimu Kocha Mkuu wa klabu hiyo Juma Mgunda ambaye amedumu na kikosi hicho kwa miezi kadhaa.

Mgunda ambaye ni kocha Mkuu wa mwezi Mei, kwa Mujibu wa TFF ambapo katika mechi 7 alifanikiwa kuipa Simba Ushindi kwenye mechi 6 na kutoa sare mechi moja dhidi ya Kagera Sugar.

Juma Mgunda aliwashinda kocha wa Yanga Miguel Gamondi na kocha Mkuu wa Azam FC Bruno Ferry ambao hawakuweza kumfikia kocha huyo kwa takwimu wa timu zao uwanjani.

Na sasa hatma ya Juma Mgunda pale mitaa ya Msimbazi, kwa habari za simba leo zinasema kwamba, Uongozi wa klabu hiyo umepanga kuachana na kocha huyo na tayari taratibu za kumsaka Kocha Mkuu atakayerithi mikoba ya Mgunda na Benchika zimeanza.

Sababu za kuachana na kocha huyo, chanzo cha habari za Simba kimeiambia Sola La Bongo kwamba, Kocha huyo amepata timu nyingine ya Ligi kuu kufundisha.

“Kocha Mgunda amepata timu moja ya Ligi kuu hapa Tanzania, hivyo tunaangalia namna ya kufanya”

Hata hivyo Soka la Bongo tunaelewa kwamba, Wagosi wa kaya Coastal Union wanamuhitaji sana Mgunda ili awe kocha mkuu wao, baada ya klabu hiyo kufuzu kucheza mashindano ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho.

Uongozi wa Simba tayari umeanza mchakato wa kutafuta kocha mwingine, na kwa sasa wametua hadi Kusini mwa Afrika kuna jina moja wanalifuatilia, mazungumzo yakikamilika na makubaliano yakienda sawa, basi Kocha Mkuu wa Simba atatoka Afrika ya Kusini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad