Hii ni Wakati Sahihi Kwa Mchezaji Clatous Chota Chama Kuondoka Simba


Hii ni Wakati Sahihi Kwa Mchezaji Clatous Chota Chama Kuondoka Simba
Mchezaji Clatous Chota Chama 

Msimu wa 2018/19 Simba SC ilikamilisha uhamisho/ usajili wa Clatous Chota Chama akitokea Lusaka Dynamos ya Zambia .

Misimu mitatu ya mafanikio akiwa na Simba ikawavutia Berkane , kama ambavyo mpira ni biashara 2021/22 Mwamba akajiunga na Berkane kutafuta changamoto mpya

2022 Mwamba akarudi tena Simba , kurudi kwake Simba hakukuwa bora sana kama awali kwa maana ya kushinda mataji hatimae msimu wa 2023/24 wamemaliza Simba ipo nafasi ya tatu NBC PL .

Chama hakuna experience mpya anayohitaji akiwa Simba , miaka 33 sasa anahitaji zaidi pesa na sio sifa na kwa maana hiyo huu ni muda /wakati sahihi wa yeye kuondoka Simba na ni wakataki sahihi pia Simba kuachana na Chama .

Tetesi zinasema kwa 51+ % Mwamba atajiunga na Yanga msimu ujao Kwa makusudi kabisa Simba wanatakiwa kuruhusu hili litokee kweli ili kujipa nafasi ya kutengeneza Simba mpya , slide ya 3 ni wachezaji waliofanya makubwa Simba lakini wakaondoka wakaiacha

Uki-swipe slide ya pili utaiona Yanga ya 2020/21 , Yanga ambayo star alikuwa Mukoko Tomombe & Niyonzima lakini kwa ajili ya kujenga Yanga bora ,kutoka kwenye hiyo line up hapo amebaki Kibwana na Mauya pekee ambao nao hawana 100% ya kuanza kwa Yanga ya sasa

Simba wasihofu juu ya tetesi pendwa ya kila msimu ambayo inaenda kuwa kweli kuelekea msimu ujao kama alivyoondoka Kagere , Lwanga na Mugalu basi waingine sokoni kutafuta bidhaa mpya na waruhusu Chama atafute changamoto mpya.

Ameandika @tariqfinest

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad