Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, amesema zoezi la kuweka kombe la ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC katika Kilele cha Mlima wa Kilimanjaro lina maana kubwa sana.
Zoezi hilo la kuweka kombe la ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC kileleni mwa Mlima Kilimanjaro lilianza Jumatano ya wiki hii.
Akizungumzia jambo hilo, Kamwe amesema: “Tumekwenda kuweka ubingwa wa Young Africans katika kilele cha mlima mrefu Afrika. Tumeiweka nembo ya ligi yetu juu ya kilele cha mlima mrefu wa Afrika, hii maana yake ni kwamba tumeiweka Young Africa kwenye kilele cha Afrika, tumeiweka ligi yetu juu kwenye kilele cha Afrika.
“Mlima Kilimanjaro ndiyo mlima mrefu zaidi Afrika, maana yake kama unaishi Bara la Asia, basi ukiichungulia Afrika cha kuanza kuona ni kombe.”
Young Africans ni mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya tatu mfululizo na ndiyo mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo kutokana na kubeba mara nyingi zaidi ambazo ni 30, anayefuatia tumemuacha mbali sana kwa makombe nane.