Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwa sasa hawatampa tena kazi kocha wa kigeni kuifundisha Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanaume 'Taifastars'.
Karia ameeleza hayo akizungumza na Mtangazaji @hoseamchopa kupitia kambi ya michezo ya @radioonetanzania.
Alipoulizwa je angependa na vilabu vya soka Tanzania viajiri makocha wazawa ?! Karia amesema angependa hata vilabu vifanye hivyo japo sio lazima.
Kuhusu idadi ya wachezaji (12) wa kigeni katika vilabu, Karia amesema anashaangaa wanaopinga kanuni hiyo kwani wachezaji wa kigeni wamesaidia ligi ya Tanzania kufanya vizuri hivyo hawafikirii kupunguza idadi.
Amesisitiza, Wanaompinga hawana DATA na TAKWIMU, ligi ya Tanzania imepiga hatua kutokana na Uongozi BORA wa (TFF).