Wakati Mashabiki wa Simba wakiwa bado wana shauku ya kutaka kujua Timu yao ina mpango gani kuelekea msimu mpya 2024/25 baada ya kutokuwa na msimu mzuri 2023/24.
Waandishi wa Habari nguli kutoka nchini wamekuja na taarifa inayoonesha hali si shwari katika Klabu ya Simba.
Mwandishi wa Habari ktoka Clouds FM, Shaffih Dauda ameandika;
Taarifa kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ni kwamba wajumbe wote wa bodi ya klabu ya @SimbaSCTanzaniakutokea upande wa mwekezaji @moodewji wamejiuzulu!
Bodi ya Wakurugenzi wa Simba inaongozwa na Mwenyekiti Salim Abdallah Muhene "Try Again"
Wakati Taarifa zikieleza hayo Mwandishi wa Habari Kutoka Kituo cha E-Fm Jemedari Said kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii ameandika;
"Mwekezaji wa Simba SC mwenye 49% Mohamed DEWJI amewapigia simu wajumbe wa Bodi ya klabu ambao wanatokana na upande wake (aliowateua yeye) na kuwataka wajiuzulu nafasi zao. Mpaka sasa wajumbe 3 wamegoma kutii AMRI ya tajiri ambao ni RASHIDI SHANGAZI,HAMZA JOHARI NA SALIM ABDALLAH