Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mfanyabiashara Mohamed Dewji ameripotiwa kutoa shinikizo la kujiuzulu nafasi zao kwa wajumbe wote aliowateua yeye ambapo mpaka sasa wajumbe watatu wamejiuzuli huku wengine watatu wakigoma.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Hamza Johari amethibitisha usiku huu kuwa naye amejiuzulu wadhifa huo.
Johari anaungana na wajumbe wengine wa Bodi ya Simba upande wa Mwekezaji Mo Dewji walioamua kujiuzulu.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Rashid Shangazi (Mbunge) amethibitisha usiku huu kuwa naye amejiuzulu wadhifa huo.
Mtu pekee anayetajwa kuwa kagoma kujiuzulu ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Salim Try Again.
"Binafsi nimeamua kujiuzulu kwasababu naona mambo hayajaenda kama tulivyotaka iwe, na nimeona nikae pembeni ili kumpa nafasi mwwekezaji ya kutafuta mtu mwingine ambaye anaweza kuisaidia Simba kurudi katika njia zake zile za kutwaa Makombe.
"Timu yoyote inayotaka kufanya vizuri lazima iwe na umoja, niwaombe Wana Simba wawe na umoja na wamwamini sana mwwekezaji.
"Mapito kwenye mpira wakati mwingine ni lazima yatokee, ziko nyakati ambazo unaweza kuwa na kila kitu lakini bado mambo yasiwe mazuri ndio maana Manchester United ya sasa sio ile ya wakati wa Ferguson, ukiuliza sababu unaweza usiipate," amesema Rashid Shangazi.