Kiungo Akataa Kujiunga Yanga Kisa Aucho na Mkude, Ahofia Kukosa Namba


Imeelezwa kuwa kiungo mkabajai wa Singida Fountain Gate, Yusuf Kagoma amekataa kusaini mkataba Yanga kutokana na ushindani wa namba ambao upo katika kikosi hicho.

Kagoma ni kati ya wachezaji waliokuwepo katika mazungumzo na Yanga, kabla ya kuchukua maamuzi ya kwenda Simba ambayo yupo katika hatua za mwisho za kumwaga wino.

Kiungo huyo ambaye aliitwa katika kikosi cha Timu ya taifa, Taifa Stars kilichoifunga Zambia bao 1-0 ugenini katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia kama angetua Yanga basi angekutana na ushindani kutoka kwa Mganda Khalid Aucho, Jonas Mkude na Zawadi Mauya wanaocheza nafasi ya kiungo mkabaji.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga, kiungo amekataa kusaini mkataba huo kutokana na ushindani wa namba uliokuwepo katika timu hiyo ambayo imepanga pia kuongeza mchezaji mwengine wa kigeni anayecheza nafasi hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad