Maskini John Bocco Apewa THANK You na Simba, Anafuata Huyu Hapa

 

Maskini John Bocco Apewa THANK You na Simba, Anafuata Huyu Hapa

Klabu ya Simba SC imetangaza kuachana na mchezaji wake na nahodha Mkuu John Bocco baada ya kutoridhishwa na mwendelezo wa ubora wake ingali John ameshakuwa kocha wa timu ya vijana ya Simba.

Nyota huyo ameitumikia Simba kwa kipindi cha miaka 7 na anakuwa wa kwanza kupewa THANK YOU katika fagio la Chuma linalotarajiwa kupita Msimbazi kwenye dirisha hili.

Kabla hata ya msimu kuisha tayari Simba, ilishambadilishia majukumu John Bocco na kumpatia timu ya Vijana ili kuwa kocha mkuu wa timu yao.

Ni utaratibu wa Simba kuwapa nafas wachezaji wao, ikiwa imefanya hivyo kwa Mussa Hassan Mgosi aliyepewa timu ya wanawake, Simba Queens.

John Bocco ni moja kati ya wachezaji wazawa wenye heshima kubwa haswa mitaa ya Msimbazi, katika ubora wake akiwa na Mnyama Simba John Aliwahi kuwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa misimu miwili.

Pia aliisaidia timu kutwaa ubingwa wa Ligi kuu bara mara nne mfululizo kuanzia mwaka wa 2017-2021, pia ameipa mataji mawili ya kombe la shirikisho FA, ikiwemo kuifikisha timu hiyo hatua ya robo fainali za kimataifa mara tano, mara 4 Ligi ya Mabingwa na mara moja Kombe la Shirikisho.

Simba wamempa heshima kubwa John Bocco,kwanza kwa kumfanya kuwa nahodha wa timu hiyo alipokuwa uwanjani, pili baada ya kiwango chake kuanza  kushuka walimshauri asomee ukocha na kisha wakampatia timu ya vijana chini ya miaka 17 ili ainoe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad