Matibabu ya Sativa Dar, Ndege Yapata Dharura Kusafirishwa Kwa Gari

 


Wakati wowote kuanzía Sasa Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa anayedaiwa kutoweka Juni 23 na kupatikana mkoani Katavi, atawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za matibabu,


Sativa alitakiwa kuwasili Dar es Salaam leo saa tisa alasiri kwa ndege maalumu ya kukodi, lakini kutokana na dharura iliyojitokeza, amelazimika kusafirishwa kwa gari la wagonjwa akitokea mkoani Dodoma kuletwa Jijini hapa.


Sativa mkazi wa Mbezi wilayani Ubungo alipatikana Alhamisi Juni 27, 2024 katika pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi akiwa na majeraha mwilini, akiomba msaada wa kupelekwa hospitalini.


Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi, Juni 29, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, mratibu wa matibabu na safari ya Sativa, Martin Masese maarufu MMM alisema Mwakabela anaendelea vema na hali yake inazidi kuimarika, ndiyo maana madaktari wametoa ruhusa asafirishwe.


Masese amesema Sativa alikuwa asafiri na Shirika la Ndege la Tanzania, tanguJuni 28 kutoka Katavi kupitia Tabora hadi Dar es Salaam, lakini kwa bahatimbaya usafiri huo ulishajaa,


Kutokana na hali hiyo, Masese amesema walishauriana na ndugu wa Sativa na madaktari na kuazimia mgonjwa huyo aletwe Dar es Salaam na gari la wagonjwa badala ya kusubiria ndege iliyopangwa kufika Dodoma usiku.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad