BAADA ya kuitumikia Yanga kwa misimu miwili kwa mafanikio sasa anatajwa kumalizana na Namungo FC kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kinataka kumaliza kwenye nafasi nne za juu msimu Ujao.
Lomalisa awali alikuwa anatajwa kujiunga Simba lakini mambo yakaenda tofauti na sasa inaelezwa Namungo inayonolewa na Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera ina mpango wa kumpa mkataba wa miaka miwili staa huyo mwenye mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Lomalisa anatajwa kuwa Moja kati ya wachezaji hodari kuwahi kucheza YANGA kwenye kipindi Cha hivi karibuni. ingawa uimara wa Nickson Kibabage Kila kukicha umempa wakati mgumu nyota huyo kuweza kung’aa.
Waziri wa Maji huyo tangu atue Yanga ameisaidia kutwaa ubingwa kwa misimu 2 mfululizo, ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikiso FA, pia kuna mashindano ya kimataifa.
Ameifikisha Yanga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, na hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Lomalisa moja kati ya mabeki wa Kikongo ambao walivyofika walikuwa na kiwango kibaya lakini, kadri siku zilivyokuwa zinaenda ndiyo kiwango chake kilizidi kupanda na akawa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha Yanga.
Lomalisa anasubiri kupewa Thank You katika kikosi hicho, ambapo hadi sasa bado hawajatangaza kuachana na mchezaji wao yeyote.