MKUTANO wa Dharula wa Wanachama wa Simba uliotakiwa kufanyika Jumamosi, Juni 15 katika ukumbi wa Gwambina umepigwa marufuku na Mamlaka za kiusalama.
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam, wamejibu barua ambayo ilitumwa na wanachama wa Simba ambao waliomba kufanya mkutano, wenye lengo la kumtaka Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu kuitisha mkutano wa dharula ili kufanya uchaguzi wa wajumbe wengine upande Ywa Wanachama.
Katika barua hiyo taarifa iliandika kwamba mamlaka za kiusalama zimekuwa na wasiwasi juu ya mkutano huo;
“Nimepokea taarifa za kiintelejesnia kuwa mkutano huo una viashiria vya uvunjifu wa amani na hauna baraka za viongozi”
“Kwa sababu za kiusalama, mkutano umezuiliwa na siyo halali, hivyo mnatakiwa kufuata taratibu za klabu ya Simba” Barua ya Jeshi la Polisi- Dar Es Salaam
Awali mashabiki na wanchama walipanga kufanya maandano ya amani na tayari kibari cha polisi kilitoka, lakini baadae inshu ikabadilika wanachama wakaona wafuate kama ambavyo katiba ya timu ya Simba inasema juu ya kufanya kikao cha matawi na wanachama wasiopungua 1000.
Baada ya kuandika barua hiyo kwenda jeshi la polisi, mchakato wa kutafuta wanachama hao ulianza, kupitia makundi ya WhatsApp na matawi ya Simba, lakini kabla ya siku husika Jeshi la Polisi wamesitisha mkutanno huo.
Hayo yote yanatokea kutokana na klabu ya Simba kushindwa kufanya vizuri kwa misimuu mitatu, huku sajili zikiwa mbovu, na makundi katika timu ni sehemu ya sababu za Simba kutofanya vizuri.