Mkuu wa Mkoa Atumbuliwa Baada ya Kudaiwa Kulawiti Binti wa Miaka 21





Dk. Yahaya Ismaili Nawanda
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Momba, Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Kihongosi amechukua nafasi ya Dk. Yahaya Ismaili Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Utenguzi wa Dk. Nawanda umekuja siku moja baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari kuwa anatuhumiwa kumuingilia kinyume na maumbile (kulawiti) binti mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu mkoani Mwanza.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Sharifa Nyanga pia imesema Rais Samia amemteua Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Kabla ya uteuzi, Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.

Rais Samia amemteua Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Magala anachukua nafasi ya Dk. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amemteua George Hillary Herbert kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi, Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa Mkuu wa Mkoa na Msajili wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Mwanahalisi online

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad