Mo Dewji Atoa Kauli Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Wajumbe wa Bodi Kujiuzulu


LICHA ya sintofahamu kinachoendelea Simba SC, Rais wa Heshima na Mwekezaji mwenza wa klabu hiyo, Mohamed 'Mo' Dewji ameibuka na kitendawili ambacho kinawaweka njia panda mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Simba imekuwa katika sintofahamu kwa kipindi cha siku tatu mfululizo, huku wajumbe wa bodi upande wa wanachama wakifichua namna wanavyopata wakati mgumu wa kuafiki mawazo ya Mo katika uwekezaji wa klabuni hapo.

Mapema leo Jumapili, Mo Dewji ameandika katika ukurasa wa instagram ujumbe unaosomeka: Kujikwa si kuanguka, bali ni kwenda mbele. Simba Tupo Pamoja!

Ujumbe wa Mo ni kama majibu ya kilichoelezwa jana Jumamosi na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Issa Masoud alifafanua kuhusu Sh20 bilioni zilizopaswa kuwekwa na mwekezaji huyo, akisema Mo anataka kugeuza fedha ambazo amekuwa akizitoa kwa klabu kama msaada kuwa deni au zigeuzwe mtaji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Masoud alisema walipokea taarifa ambazo hazikuwa katika urasmi wake ikiwataka kama bodi kupitisha azimio lililokuwa likisema pesa alizokuwa anazitoa mwekezaji kama msaada zihesabiwe katika hisa.

Hata hivyo, ujumbe wa Mo Dewji ulipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo wengine wakimuunga mkono kwa kaulio hiyo wakisema wapo pamoja naye na wengine wakimpiga 'dongo' kiaina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad