Molinga: Kwa Kosi lile, Chama Atakosa Namba Yanga

 

Molinga: Kwa Kosi lile, Chama Atakosa Namba Yanga

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, David Molinga amesema kuwa uamuzi alioufanya kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chota Chama wa kutimkia Yanga ni uamuzi sahihi kwa sasa kwani utamfanya kurejesha makali yake aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma.


Molinga ambaye ni raia wa Congo DR amesema kuwa Chama anayo kazi kubwa ya kwenda kupambania namba kwenye kikosi cha kocha Miguel Gamondi kwani kwenye nafasi anayocheza wapo wachezaji wengi ambao wanafanya vizuri.


“Kwenda Yanga sio mbaya lakini anatakiwa aoneshe sana kwa sababu kupata nafasi sio rahisi. Sasa hivi kila mtu anaweka kikosi chake kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu wanataka kwanza asaini mkataba, sasa kusaini mkataba na kucheza ni vitu viwili tofauti. Kusaini ndiyo tunakutaka lakini kucheza kwenye kikosi cha kwanza ni wewe mwenyewe.


“Chama ni mchezaji mzuri na mimi naelewa amekaa sana Simba wakati mwingine unazoeleka watu wanakuona ni wa kawaida lakini yeyey mwenyewe anaona abadilishe mazingira, kwangu ninaona ni vizuri lakini pale Yanga ajue sio rahisi kupata nafasi kirahisi kama alivyokuwa Simba kwamba mashabiki wanaimba kocha muweke Chama.


“Pale aweke kichwani mwake kwamba anakwenda kwenye timu ambayo ina wachezaji wazuri kwenye nafasi anayocheza. Kusaini ni viongozi na kocha anakutana lakini kucheza ni wewe mwenyewe. Kucheza Yanga ni nzuri sana kwake hata Simba ilikuwa nzuri lakini kufanya mabadiliko ni mbaya anaweza kurudi kwenye ubora wake ambao watu walimzoea.


“Wachezaji wanapokuwa wengi kwenye nafasi moja hilo ni jambo zuri kwa sababu kikosi kinakuwa kipana na kumpa kocha nafasi ya kuchagua nani aanze nani apumzike au kufanya rotation kutokana na mpango kazi wa mwalimu kuelekea mechi husika. Michuano ni mingi lazima wachezaji wapeane nafasi lakini ubora wa kikosi na kuwe na uhakika wa kupata matokeo.


“Mbappe amefanya kila kitu na PSG lakini ameamua kwenda Madrid ili akafanye kitu cha tofauti kwa hiyo hata kwa Chama ni hivyo. Yanga wamefanya jambo jemba kwa sababu wanaboresha kikosi chao tumeona hata CAFCL wanacheza na Memelodi, bori linatembea Yanga wanapiga pasi za kutosha,” amesema Molinga.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad