DAR ES SALAAM; LUIS Miquissone amesema safari yake katika soka la Tanzania imefi ka mwisho baada ya kumaliza mkataba wake na Simba.
Miquissone aliyejiunga na Simba baada ya kuvunja mkataba wake na Al Ahly ya Misri dirisha kubwa la usajili la msimu wa mwaka 2023/24, aliachwa na Wekundu hao wa Msimbazi sambamba na John Bocco, Saido Ntibazonkiza, Shabani Chilunda na Kennedy Juma.
Nyota huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Ud Songo ya Msumbiji kwenye mahojiano ya video fupi aliyotuma kwenye akaunti yake ya Instagram, alisema hana mpango wa kucheza soka Tanzania baada ya kuachana na Simba.
“Siwezi kuishi Tanzania, safari yangu Tanzania imefikia mwisho, huo ndio ukweli,” alisema Miquissone akiwa nyumbani kwao Msumbiji. Aliongeza: “Mashabiki wa Simba watakuwa moyoni mwangu daima, kwenye mpira wa miguu ni kawaida kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine”.