P Diddy Apokonywa Shahada ya Heshima Kutoka Chuo Kikuu cha Howard



Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali inazidi kuwa mbaya kwa Rapa Diddy na hii imekuja mara baada ya Chuo Kikuu cha Howard kilichopo nchini Marekani, kutangaza hivi karibuni kumvua Shahada ya heshima waliyomtunuku mwaka 2014. Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya makubaliano ya bodi ya wadhamini ya chuo hicho.

Chuo kikuu cha Howard kiliripoti ya kwamba, bodi yake ya wadhamini ilipiga kura kwa kauli moja kurejesha Shahada “Degree” waliyompatia rapa Diddy kufuatia kutolewa kwa video ya mwaka 2016 iliyomwonesha akimshambulia mpenzi wake wa zamani, Cassie Ventura. Taarifa ya chuo hicho inasema kitendo kilichoonekana kwenye video hiyo hakiendani kabisa na maadili na imani ya chuo hicho na hafai kabisa kuwa na heshima hiyo ya juu kabisa.

Taarifa ya bodi ya wadhamini pia ilibainisha kuwa chuo kitasitisha makubaliano ya zawadi ya Diddy ya mwaka 2016 na kufuta udhamini ambao ulikuwa umeanzishwa kwa jina lake, kurudisha mchango wake wa (USD 1M) na kufuta makubaliano ya ahadi ya mwaka 2023 na Sean Combs Foundation dhidi ya chuo hicho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad