PAUL Makonda aagiza Wakuu wa idara sita wahamishwe Arusha

 

PAUL Makonda aagiza Wakuu wa idara sita wahamishwe Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ameagiza kuhamishwa kwa Wakuu wa Idara mbalimbali za Mkoa wa Arusha ambao wamehudumu kwenye Mkoa huo kwa zaidi ya miaka mitano.


Waliohamisha kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ni pamoja na James Labikoki ambaye ni Afisa usafirishaji na taka ngumu, Theresia Maro ambaye ni Afisa TEHAMA, Mfaume Mfaume Afisa Utumishi na Dkt. Onesmo Mandike ambaye alikuwa Afisa Kilimo na Mifugo.


Mkuu wa Mkoa pia ametoa maagizo kwa Katibu tawala wa Mkoa Mussa Missaile kuwashusha vyeo Yusuph Mange aliyekuwa Afisa Elimu Sekondari na Hussein Bakari Afisa Elimu Msingi ambao wanadaiwa kushindwa kutimiza majukumu yao kikamilfu na hivyo kuathiri usimamizi wa miradi ya elimu.


Mkuu wa Mkoa amefikia hatua hiyo mara baada ya kumtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Injinia Juma Hamsin kumueleza kuhusu wanaokwamisha mambo ya Halmashauri kusonga mbele ambapo katika maelezo yake alimuomba Mkuu wa Mkoa kuwahamisha Watumishi waliofanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano kwenye kituo hicho kimoja cha kazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad