Polisi Wamshikilia RC wa zamani wa SIMIYU kwa Kumlawiti Mwanafunzi

 

Polisi Wamshikilia RC wa zamani wa SIMIYU kwa Kumlawiti Mwanafunzi

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC) Dk Yahya Nawanda kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa Chuo Kikuu kimojawapo jijini Mwanza.


Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Nawanda imetolewa leo Alhamisi Juni 13,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa.


Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, Jeshi hilo linaendelea kumshikilia Dk Nawanda kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma hizo huku uchunguzi wa kina ukiendelea kuhusiana vielelezo vya tukio hilo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitengua uteuzi wa mkuu huyo wa mkoa Juni 11, 2024.


Rais Samia alimteua aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Momba, mkoa wa Songwe, Kenan Kihongosi kuchukua madaraka hayo ya ukuu wa mkoa wa Simiyu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad