Rais Mwinyi agoma kuongezewa muda wa kuongoza Zanzibar

 

Rais Mwinyi agoma kuongezewa muda wa kuongoza Zanzibar

Ikulu ya Zanzibar kupitia kwa Mkurungenzi wa Mawasiliano, Charles Hilary imepinga suala la Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuongezewa muda wa kukaa madarakani, huku ikisisitiza maoni hayo sio yake.


Taarifa hiyo iliyotolewa leo Jumatatu Juni 24, 2024 imeeleza;


“Hivi karibuni kumetolewa maoni yanayopendekaza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar.


“Maoni hayo yamekwenda mbali zaidi hata kutaka uchaguzi mkuu wa mwakani kumchagua Rais wa Zanzibar usifanyike, jambo hili halina tija wala faida kwa nchi yetu na Chama cha Mapinduzi (CCM) chenye kufuata misingi ya demokrasia,” imeeleza taarifa hiyo.


Pia, taarifa hiyo imeeleza ; “Rais Dk Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na sheria za nchi, tunapenda kusisitiza kwamba maoni haya si ya Rais wala sio ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.


“Kwa muktadha huu, Rais Dk Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Aidha, amewasihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo,” imeeleza taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imetolewa, siku moja tangu, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohamed Said Dimwa wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Dimami kusema; “Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalumu kuridhia kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuongoza nchi katika muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano.”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad