Rais Samia Afunguka "Natukanwa SIJIBU Nimejigeuza Chura"

 

Rais Samia Afunguka "Natukanwa SIJIBU Nimejigeuza Chura"

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amesema anayasikia matusi anayotukanwa lakini amejigeuza chura anajifanya hasikii na wala hatojibu bali anachotaka yeye ni mageuzi ya kiuchumi ili kuipeleka Nchi ya Tanzania mbele.


Akiongea leo June 11,2024 wakati wa akipokea gawio na michango kutoka Mashirika na Taasisi za Umma Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Samia amesema “Kwenye mageuzi haya Mchechu na Waziri wako lazima muwe unpopular, sijawahi kusikia Waziri wa Fedha akasifiwa hata siku moja, siku zote Waziri wa Fedha analaaniwa, kwahiyo Mchechu na wewe utalaaniwa tu hapa, na nyingine zitakuja personal nyingine kikazi lakini hii ndio kazi niliyokupa simama na ifanye”


“Mimi kazi mliyonipa nasimama na naifanya, na mnashuhudia matusi ninayotukanwa ‘Mpuuzi, hana maana, huyu Bibi , eeh eeh ana hivi!’ mambo tele lakini najigeuza chura kelele zinapigwa nyingi wakiona haujibu wanasema sasa tulitukane litajibu au lijibu, sijibu najigeuza chura masikio sisikii kabisa ninachotaka mageuzi ya kiuchumi ndani ya Nchi hii, anayetaka kunikere anikanyagie uchumi wangu”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad