Rashid Shangazi Afunguka Sababu za Kujiuzulu SIMBA, Amtaja Mo Dewji

 

Rashid Shangazi Afunguka Sababu za Kujiuzulu SIMBA, Amtaja Mo Dewji

Mbunge wa Jimbo la Mlalo na aliyekuwa mjumbe kamati ya bodi ya wawekezaji wa Simba SC kupitia upande wa mwekezaji Mohamed Dewji “MO”, Rashid Abdallah Shangazi ameeleza sababu ya kujiuzulu kwake kwenye nafasi hiyo.

Shangazi amesema kuwa ameamuandikia Mohamed Dewji, barua ya kumuomba kujiondoa kwenye bodi ya uwekezaji tangu Juni 2, 2024 hii ni kutokana na mwenendo mbaya wa timu ya Simba SC.

“Kati ya mambo yaliyonifanya nijiuzulu ni kupisha mwekezaji kutengeneza safu mpya ya bodi itakayoisaidia klabu yetu kwani hatukuwa na matokeo mazuri kwa kipindi cha misimu miwili hivyo nimefanya hivi kama sehemu ya uwajibikaji,” amesema Shangazi.

Amesema kuwa mwenendo mbaya wa timu yao umemfanya kupisha mwekezaji kutafuta watu wengine watakaoifikisha timu sehemu nzuri kama awali.

Shangazi amewataka wanachama na mashabiki kwa kuwa karibu zaidi na uongozi haswa katika kipindi hiki cha mapito.

“Uongozi ni kupokezana na unahitaji mshikamno na nguvu ya pamoja, msiiaache timu, sisi tumewajibika ili tujipange upya na tutaendelea kutoa michango yetu kadri itakavyohitajika,” amesema Shangazi.

Taarifa zilizotufikia mida hii ni kwamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Salim Abdallah Try Again, aliyesemekana ni miongoni mwa wajumbe waliojiuzulu, hakuna kitu kama hicho na kiongozi huyo yupo sambamba na muwekezaji MO Dewji nje ya nchi, wakijadiliana namna ambayo itawafanya kuja kivingine na Simba mpya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad