Tangu kuanza kwa mchakato wa uwekezaji ndani ya Simba miaka imepita na utaratibu wa uendeshaji wa klabu umebadilika sana
Asilimia 49% ambayo ni sehemu ya uwekezaji ndani ya Simba kama inavyoelekezwa na serikali wanatakiwa kuwa wawekezaji watatu na sio muwekezaji mmoja tena
Lakini pia watu wanapaswa kujua kuwa thamani ya Simba imebadilika sio bilioni 20 tena,inapaswa kuwa zaidi ya hapo
Mimi binafsi Mo simuiti muwekezaji kwa sasa ila ni mdau wa michezo au mfadhili wa Simba hivyo basi na yeye anapokuja na hoja ya kudai pesa zake alizotoa na yeye asikilizwe kwa sababu mchakato haujakamilika