Silaa Apiga Marufuku mabango ya Uuzaji wa Viwanja mitaani

 

Silaa Apiga Marufuku mabango ya Uuzaji wa Viwanja mitaani

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amepiga marufuku nchi zima mabango yaliyozagaa mitaani ya kuuza viwanja maarufu viwanja vinauzwa na ametoa siku 7 kwa maafisa ardhi nchi nzima kuhakikisha mabango hayo yanaondolewa na ameagizo pia makampuni yote yanayouza viwanja kuweka dawati la mauzo ofisi za ardhi za wilaya na mikoa.


Silaa ametoa maagizo hayo katika ofisi za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam alipokuwa akisikiliza kero za wananchi waliofika kutafuta haki zao baada ya kuuziwa viwanja hewa na kampuni ya Digital Auction LTD kwenye eneo ambalo hawalimiliki katika Manispaa ya Kigamboni na kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 166.


“Huwezi kuuza kiwanja kwa ramani, kiwanja kinauzwa kwa hati, Serikali haiwezi kukaa kimya wakati wananchi wanyonge wanateseka na kutapeliwa fedha zao” Amesema Waziri Silaa.


Aidha, amewataka Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa yote nchini kuharakisha mchakato wa utoaji wa hati kama zao la upimaji wowote wa ardhi na amewataka wenye makampuni ya ardhi wanaotaka kuuzia viwanja maofisini mwao waombe hati za viwanja wanavyopima.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad