Taarifa ya Polisi Kuhusu Kijana SATIVA aliyetekwa na Kupatikana Katavi Akiwa Hoi




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani, ameongelea kuhusiana na tukio la kupotea na kupatikana kwa Edgar Mwakabela (SATIVA) ambapo amesema "Ndio ni kweli, taarifa za tukio hilo lipo na tayari tumeshaenda eneo la tukio na Mgonjwa sasa hivi yupo Hospitali ya Wilaya ya Mlele anaendelea na Matibabu
-
SACP Ngonyani amesema Uchunguzi wa awali umebaini #Sativa aliokotwa na Wasamaria wema Usiku wa Kuamkia Juni 27, 2024 Barabarani maeneo ya Pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi (Barabara ya Mpimbwe Majimoto inayoelekea Mpanda)

pia mgonjwa mwenyewe ameongea japo kwa shida akasema alikamatwana watu wasiojulikana juni 23 Mbezi kwa Msuguri kisha wakampeleka mkoani Arusha katika sehemu ambayo haijui na baadae kupelekwa katavi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad