Taifa Stars Ikishinda Leo Dhidi ya Zambia Itapanda Nafasi ya Pili




Leo kuna mechi mbili za kundi E
Zambia 🇿🇲 vs 🇹🇿 Tanzania
Congo vs 🇲🇦 Morocco

Kundi hili linaongozwa na Morocco wenye alama 6 , kwenyenafasi ya pili yupo Zambia akiwa na alama 3 sawa na Niger aliye nafasi ya tatu na Tanzania nafasi ya nne wote wakiwa na alama 3.

Mchezo kati ya Zambia na Tanzania , Zambia anapewa nafasi kubwa ya kushinda kihistoria na faida ya uwanja wa nyumbani lakini viwango vya timu hizi kwa sasa havipishani sana .

Mara ya mwisho kwenye AFCON ,Zambia wao ndio walichomoa dakika za jioni kabisa hivyo mchezo upo wazi na yoyote anaweza kupata ushindi .

Bila kujali matokeo ya Congo na Morocco, Tanzania ikishinda mchezo wa leo saa 1:00 usiku itapanda hadi nafasi ya pili na kama itapata idadi kubwa ya magoli na Morocco atapoteza saa 4:00 usiku basi Stars inaweza kuongoza kundi ingawa option ya pili ni ngumu kwa aina ya mpinzani [ Zambia ]

Kila la kheri Taifa Stars 🇹🇿

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad