Tanzia: Mtangazaji Swedy Mwinyi afariki Dunia

 

Tanzia: Mtangazaji Swedy Mwinyi afariki Dunia

Mtangazaji mahiri wa vipindi wa michezo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Sued Mwinyi amefariki Dunia juzi Mei 12, 2024 katika hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.


Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dk. Ayub Rioba Chacha amethibitisha kutokea kwa msiba huo.


Mwinyi atakumbukwa kwa umahiri wake wakati wa matangazo ya mpira wakati ule akitangaza kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadaye TBC.


Pia amewahi kufanya kazi na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW). Mara ya mwisho ameonekana #mjengoni Aprili 2020 kwenye Jaramba la Wikiendi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad