Uhuru Kenyetta Afunguka Sakata la Maandamano Kenya : Nawaunga Mkono Wananchi



Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyetta ametoa wito wa kupatikana kwa utulivu na amani kurejeshwa kufuatia maandamano makubwa Nchini humo na kuwataka Viongozi kutambua kuwa madaraka na mamlaka waliyonayo wamepewa na Wananchi hivyo kuwasikiliza Watu ni lazima na sio jambo la hiari.

Kenyatta ameutaka pia Uongozi kuchukua uamuzi sahihi wa kusikiliza na kutowapuuza Watu akisema vurugu kwa pande zote mbili sio suluhisho la matatizo ———> “Wapendwa Wakenya nasimama nanyi na naomba Uongozi uzungumze na Wananchi, naomba amani na maelewano kwa kila Mkenya na sote tukumbuke Kenya ni kubwa zaidi kuliko mmoja wetu”

“kama Rais wenu wa zamani nimeona uzito na ugumu wa kuiongoza Kenya, kwahiyo ninaomba hekima na ustaarabu uimarishwe na amani na maendeleo iwe kwetu sote Watoto wa Kenya" ——— Mstaafu Uhuru Kenyatta

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad