USAJILI: Aziz K Kutimkia TIMU ya Mayele, Simba Wamkataa LIVE Lomalisa
WAKATI Yanga wakipambana kumbakiza, Stephane Aziz Ki ambaye ndiye kinara wa upachikaji wa mabao msimu huu (21) inaelezwa Pyramids FC ya Misri imeonyesha nia ya kumuhitaji staa huyo.
Yanga na Aziz Ki walithibitisha kuendelea kupiga kazi pamoja, japo bado hajasaini mkataba na Pyramids imetuma ofa.
Akiondoka klabuni hapo, anaenda kujiunga na aliyekuwa mshambuliaji namba moja wa timu ya Yanga, Fiston Mayele ambaye alisajiliwa msimu ulioisha.
Aziz ki amekuwa na kiwango kizuri sana akiwa na Yanga kwa misimu yote miwili, huku msimu uliomalizika akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC, huku akiisaidia timu yake kutwaa taji la 30 la Ligi, na Kombe la Shirikisho la CRDB.
Kwa upande wa Simba, wao wametua hadi DR Congo kwenye klabu ya FC Lupopo, ambapo wanafanya mazungumzo na beki wa kushoto Valentin Nouma, amabaye ni mbadala wa Joyce Lomalisa aliyekuwa akinyapiwa na Mnyama Simba.
KIUNGO mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Mghana Christian Zigah huenda msimu ujao asiwe sehemu ya kikosi hicho baada ya kumaliza mkataba. Hakuna mazungumzo yanaendelea baina ya Dodoma na Zigah na tayari kiungo huyo wa zamani wa Biashara United aliyemaliza msimu ulioisha akifunga mabao matatu na ameondoka Dodoma akiwa safarini kurudi Ghana.
KIUNGO mkabaji aliyemaliza mkataba na KMC, Masoud Abdallah ‘Cabaye’, ameingia katika rada za maafande wa Mashujaa na Tanzania Prisons, wanaohitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano. Imeelezwa mchezaji huyo, anaangalia ni timu gani itakuwa na masilahi yatakayomridhisha kisha akasaini.